Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi zaibeba Simba, KMC

75571 Pic+simba

Fri, 13 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

LEO Ijumaa jioni kutakuwa na michezo miwili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, mabingwa watetezi Simba watakuwa nyumbani kuikaribisha Mtibwa Sugar uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam  wakati Coastal Union wao wanaikaribisha KMC uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Rekodi zinaonesha misimu mitano ambayo Mtibwa Sugar imekutana na Simba katika mechi 10 haijawahi kushinda mechi hata moja iwe uwanja wa Uhuru au Jamuhuri Morogoro.

Msimu uliopita mechi mbili Mtibwa Sugar mchezo wa kwanza wakiwa ugenini walikubali kufungwa mabao 3-0, huku ule wa marudiano uliopigwa uwanja wa Jamuhuri, Mei 16 mwaka huu walitoka suluhu siku ambayo mabingwa wa ligi walikadhiwa kombe lao.

Msimu wa 2017/18, mchezo wa kwanza ulimalizika kwa sare 1-1, wakati ule wa marudiano Simba walishinda bao 1-0, bao lililofungwa na Emmanuel Okwi ambaye kwa sasa hayupo katika kikosi hicho.

Msimu wa 2016/17, mechi ya kwanza Simba walishinda mabao 2-0, wakati ule wa marudiano ulimalizika kwa suluhu.

Ubabe wa Simba haukishia hapo kwani msimu wa 2015/16, mechi ya kwanza walishinda bao 1-0, kama ambavyo walivyofanya mchezo wa pili uliochezwa Mai 15, Mtibwa wakiwa nyumbani walikubali kufungwa tena bao 1-0.

Msimu wa 2014/15, mechi ya kwanza Mtibwa Sugar wakiwa ugenini walitoka sare 1-1, wakati mchezo wa marudiano uliochezwa Machi 14, Simba wakiwa ugenini waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Katika mechi ya leo, rekodi za misimu mitano zinaonekana kuibeba Simba katika mechi 10 wameshinda sita na hawajapoteza wowote huku mechi nne zikiisha sare kwa maana zilimalizika bila ya kuwepo mbabe.

Simba katika mechi zote 10 wamefunga mabao 11, wakati wao nyavu zao zikikubali kutikiswa kwa maana ya kufungwa mabao mawili tu.

Kikosi cha Simba mbali ya kuonekana rekodi kuwabeba mpaka katika mazoezi ya mwisho ambayo walifanya jana Alhamis uwanja wa Uhuru walimkosa straika wao Meddie Kagere ambaye aliwasili usiku akitokea Rwanda kwenye majukumu yake ya timu ya Taifa.

Benchi la ufundi la Simba katika mazoezi yao ya kucheza walilazimika kuwatumia Sharaf Eldin Shiboub, Miraji Athumani, Rashid Juma na Cletous Chama katika safu ya ushambuliaji ingawa wote kiasili si nafasi yao.

Matokeo hayo yanaonesha kuwa Simba wanaingia katika mchezo huu wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar wakiwa na rekodi nzuri ambazo zinawabeba.

KMC, COASTL UNION MKWAKWANI

Mchezo mwingine wa ligi, ni kati ya wenyeji Coastal Union ambao wapo uwanja wa nyumbani wa CCM Mkwakwani Tanga ambapo watacheza dhidi ya KMC.

Union wao mechi ya kwanza walipoteza kwa kufunga na Polisi Tanzania bao 1-0, wakiwa ugenini, wakati KMC wenyewe walifungwa bao 1-0 dhidi ya Azam.

Rekodi zinaonesha timu hizi mbili zote zilipanda daraja msimu uliopita huku mechi ya mzunguko wa kwanza Coastal Union wakiwa nyumbani walitoka sare 1-1, wakati mechi ya marudiano iliyochezwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, KMC ilishinda mabao 5-2.

Chanzo: mwananchi.co.tz