Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi za mita 100 wanawake Olimpiki

GriffithJoyner Cover.jpeg Rekodi za mita 100 wanawake Olimpiki

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashindano ya Olimpiki yanatarajiwa kuanza Julai 26 mwaka huu kwenye jiji la Paris nchini Ufaransa.

Haya ni mashindano makubwa na yenye heshima kubwa kwa miaka mingi na mwaka huu wanamichezo mbalimbali wanayasubiri kwa hamu kubwa sana.

Pamoja na mashindano mengine, lakini riadha ni kati ya yale ambayo yamekuwa yakiwavutia watu wengi zaidi kwa miaka mingi ukiwa pia ndiyo mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa mwaka huu.

Mbio za mita 100 zimekuwa zikitoa wanariadha wapya kila mwaka ambao mashindano hayo yamekuwa yakifanyika lakini kuna rekodi moja ambayo inashikiliwa na mwanariadha Florence Griffith-Joyner ambayo imedumu kwa miaka mingi.

Rekodi ya mwanariadha huyo ndiyo gumzo kwenye mashindano haya mwaka huu na kila mmoja anayekimbia mita 100 amekuwa akisema kuwa anataka kwenda kuivunja.

Florence mwaka 1988, aliweka rekodi ya kutwaa medali ya dhahabu kwa kukimbia kwa sekunde 10.49 na hadi leo hakuna mwanariadha mwingine ambaye amefanikiwa kuifikia pamoja na kwamba imepita misimu kadhaa ya Olimpiki.

Kwa kipindi cha mashindano matano ya Olimpiki kila mwanariadha wa kike aliyetwaa medali kwenye mbio za mita 100 ameshindwa kuifikia rekodi hiyo.

Waliowahi kuikaribia ni wale wa mwaka 2004 ambao walikimbia kwa sekunde 10.93 huku 2021 mwanariadha akitwaa medali hiyo kwa kukimbia kwa muda wa 10.61 mwaka 2021.

Hata hivyo, rekodi hiyo ya Griffith-Joyner imekuwa ikitajwa kuwa imejaa utata mkubwa kwa sababu moja kuu.

Inaelezwa kuwa kulikuwa hakuna utaratibu wa kupimwa kama mwanariadha ametumia dawa za kusisimua misuli wakati huo jambo ambalo wengi wanaamini kuwa mwanariadha huyo inawezekana alizitumia.

Hata hivyo, hakuna udhibitisho wa kutosha kwenye hili.

Kabla Griffith-Joyner hajaweka rekodi hii mwanamke ambaye alikuwa anaishikilia alikuwa Evelyn Ashford ambaye alikimbia kwa muda wa sekunde 10.79 mwaka 1984.

Nafasi ya pili inashikiliwa na Mjamaica Elaine Thompson-Herah, ambaye alikimbia kwa sekunde 10.54 kwenye mashindano hayo yalifanyika Tokyo Japan mwaka 2021 ambaye bado amefuzu kwenye mbio za mwaka huu jijini Paris.

"Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa najiuliza kama naweza kuvunja rekodi yangu ambayo nimewahi kuiweka, lakini naamini kwamba sasa ni muda sahihi sana,” alisema.

Rekodi ya nafasi ya tatu inashikiliwa pia na mwanariadha raia wa Jamaica, Shelly-Ann Fraser-Pryce ambaye naye atakuwepo kwenye mashindano ya mwaka huu akiwa alikimbia kwa muda wa sekunde 10.60 mwaka 2021, kwa sasa ana umri wa miaka 37 na haya yatakuwa mashindano yake ya mwisho.

"Nitakwenda Paris nikiwa na nguvu ya kutosha baada ya kujiandaa vyema, lakini nafikiri haya yatakuwa mashindano yangu ya tano ya Olimpiki na yatakuwa ya mwisho.

“Sina shaka hata kidogo na uwezo wangu naamini kwenye kupambana na hilo ndiyo jambo ambalo limekuwa likinibeba kwenye maisha yangu yote nitafanya kila kitu kulingana na uwezo wangu unavyotaka,” alisema.

Chanzo: Mwanaspoti