Mshambuliaji wa AC Milan, Zlatan Ibrahimovic alifikisha bao lake la 400 katika Ligi Kuu wakati timu yake ikishinda bao 2-1 dhidi ya AS Roma.
Zlatan mwenye umri wa miaka 40 alifunga bao na kusababisha penati iliyofungwa na Frankie Kessy huku la AS Roma likifungwa na El Shaarawy.
Nyota huyo wa Sweden amecheza Ligi Kuu mbalimbali ikiwemo Ligi ya Hispania, Ufaransa, Uholanzi.
AC Milan imekuwa timu ya nne kushinda mechi 10 kati ya 11 za mwanzo kama walivyofanya Napoli msimu huu(mara mbili), Juventus (mara mbili) na AS Roma.
Ushindi wa jana, umewafanya AC Milan kufikisha alama sawa na Napoli ambao walishinda bao 1-0 Salerlitana na sasa wana alama 31.