Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi ya mabao mengi iliyowekwa Kombe la Dunia

8921 MABAO+PIC TZW

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kutana na rekodi ya mabao mengi yaliyowekwa kwenye historia ya fainali za Kombe la Dunia tangu zilipoanzishwa mwaka 1930.

Mechi ya Austria dhidi ya Switzerland hatua ya robo fainali iliyopigwa Juni 26 1954. Austraria iliibuka na ushindi wa mabao 7-5 dhidi ya Switzerland.

Pia Brazil iliifumua Poland mabao 6-5 kwenye hatua ya kwanza ya makundi Juni 5 mwaka 1938.

Hungary iliilima Ujerumani mabao 8-3 kwenye kundi B Juni 20, 1954.

Hungary ilirudia kutoa kichapo kikali tena fainali za mwaka 1982 ikiiliza El Salvador mabao 10-1.

Nayo Ufaransa ilifanya mauaji Juni 8, 1958 kwenye Kundi la 2 ambapo iliifumua Paraguary mabao 7-3 yaliyofungwa ndani ya dakika 90.

Huko nao Argentina iliitibua nyongo Mexico 19 Julai, 1930 kwenye kundi lao la kwanza kwa kuifanyia kitu mbaya nchi hiyo ikiibua na ushindi wa mabao 6-3.

Hungury ilifanya mauaji mengine 17 Juni 1954 ikiilamba Jamhuri ya Korea mabao 9-0 ambayo ilishinda mabao yote ndani ya dakika 90.

Ujerumani iliishindilia Uturuki mbao 7-2  tarahe 23 Juni 1954 kwenye kundi lake la 2. Mabao yote yalitinga wavuni ndani ya dakika 90.

Ufaransa iliichezesha tena kwata Ujerumani kwa kugawa kichapo cha mabao 6-3 28 Juni mwaka 1958.

Yugoslavia walitoa kipigo cha mbwa mwizi kwa Zaire ambayo sasa ni Congo DR 18 Juni 1974 kwenye kundi la 2, ikiifunga mabao 9-0.

Chanzo: mwananchi.co.tz