Klabu ya Manchester United imefikia makubaliano na kocha Ralf Rangnick kwa ajili ya kuinoa timu hiyo kwa miezi sita, akichukua nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer aliyefukuzwa wiki iliyopita.
Taarifa zimeripoti kwamba mabosi wa Man United wamefanya mawasiliano na Lokomotiv Moscow ili kumruhusu Rangnick kuachia nafasi yake ya Ukuu wa Maendeleo wa Michezo wa klabu hiyo.
Rangnick, ambaye sasa ana miaka 63, amesaini mkataba wa miaka sita wa kuinoa Man United, lakini mazungumzo mengine ni kwamba kocha huyo anataka kupewa majukumu mengine ya uongozi kwenye klabu hiyo.
Hata hivyo, Man United bado haijafikia makubaliano huku mabosi wa Man United wana imani dili hilo litakamilika baada ya mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea, utakaocheza kesho. Endapo kama dili hilo halitakamilika Michael Carrick ataiongoza timu hiyo kuelekea mchezo huo.
Rangnick anafahamika kama profesa wa mpira nyayo zake zikifutwa na Thomas Tuchel, Jurgen Klopp and Julian Nagelsmann, ingawa kocha huyo hajawahi kufundisha timu nje ya Ujermani, amefanikiwa kuinoa RB Leipzig kwa asilimia 55 akiisaidia timu hiyo kupanda ligi ya Bundesliga msimu wake wa kwanza na alianza nayo kuanzia msimu wa 2015 hadi 20-16 na 2018 -2019.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Man United ilichagua makocha watano ambao wanapewa mafasi ya kubeba mikoba ya Solskjaer akiwemo Rangnick kabla ya kocha mpya kuteuliwa msimu ujao, makocha hao ni Ernesto Velverde, Lucien Favre, Rudi Garcia, Paulo Fonseca.
Rangnick ni nani?
Rangnick akijulikana kama muasisi wa soka la kuanza kushambulia baada ya kupokonywa mpira, Rangnick anatajwa pia kama kocha mwenye uwezo mkubwa wa kusoma mchezo haraka.
Anatajwa kama ndiye aliyawashawishi na kuwapa mafanikio makocha Jurgen Klopp, Thomas Tuchel na yuler wa Bayern Munich, Julian Nagelsman.
Akijulikana kwa jina la utani la ‘The Professor’, aliheshimika zaidi kwa aina yake ya ufundishaji liitwalo ‘Gegenpressing’, ambalo linajulikana kwa ukabaji wa kasi wa kuanzia nusu ya pili ya wapinzani.
Hilo limeonekana kuwa na faida kiasi cha makocha wengi wa sasa kuanza kuiga utaratibu huo. Kwa mshangao, rangnick alianza kuwa kocha wa soka akiwa na miaka 25, wakati huo ilikuwa 1983.
Aina yake ya ufundishaji ilikuwa tofauti, kiasi cha hata timu ya taifa ya Ujerumani kuanza kutumia mfumo wa 3-5-2, ambao hata sasa unatumiwa na makocha wengi, ukifanana na ule wa Tuchel, wa 3-4-2-1.