Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ramadhan Brothers wadondokea pua Marekani

Ramadhani Brothers 5.jpeg Kundi la Wanasarakasi la Ramadhani Brothers kutoka Tanzania

Thu, 28 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la Wanasarakasi la Ramadhani Brothers kutoka Tanzania wamemaliza katika nafasi ya tano kwenye shindano maarufu la Kusaka Vipaji la 'America's Got Talent' lililofanyika nchini Marekani.

Ramadhani walionesha Sanaa yao ya kushangaza mbele ya majaji wanne akiwemo Simon Cowell, Sofia Vergara, Heidi Klum na Howie Mandel ambapo Adrian Stoica ndiye aliyeibuka mshindi.

Kupitia ukurasa wao wa mitandao ya kijamii Ramadhani Brothers wameandika "Hatujapata kura za kutosha, tumekuwa watano katika shindano, na tunashukuru AGT kwa nafasi hii na watu wote waliotupigia kura, mapambano yanaendelea"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live