Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Shirikisho la kuogelea duniani kutembelea Zanzibar

Rais Pic Rais wa Shirikisho la kuogelea duniani kutembelea Zanzibar

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Rais wa Shirikisho la Kuogolea Duniani (Fina), Husain Al Musallam anatarajia kuwasili Zanzibar kesho Jumanne Machi 15, 2022 katika ziara yake ya siku mbili kisiwani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Machi 13, 2022 kuhusu ujio wa rais huyo atakeyeongozana na ujumbe wa watu 25, Balozi wa heshima wa Brazili Zanzibar,  Abdulsamad Abdulrahim amesema baada Rais huyo kuwasili atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi Ikulu, Zanzibar.

“Ziara ya Rais wa Fina Zanzibar itakuwa ya kwanza kwa ofisa Mkuu wa Fina kuzuru nchi hiyo tangu Tanganyika ilipopata uhuru wake mwaka 1961,” amesema Abdulsamad

Ameseme lengo la ziara hiyo ni kujadili na kutathmini maendeleo ya baadaye ya kuogolea kwa ushindani Zanzibar, pia atafanya mazungumzo na viongozi na wadau wa mchezo huo namna unavyoweza kuendelezwa kisiwani humo.

“Atazungumza na waogeleaji wadogo, makocha na wadau wengine kuhusu uzoefu wao wa maisha kama wanariadha wa ngazi za juu na atatembelea waogeleaji vijana wadogo katika shule ya International School Zanzibar Mazizini,” amesema

Ziara hiyo inafanyika ikiwa Zanzibar inajipanga kujenga bwawa kubwa la kuogolea lenye hadhi ya olimpiki linalokadiriwa kugharimu dola za kimarekani milioni 3 (Sh6.9 bilioni) ili kuwawezesha vijana wanaofanya mchezo huo kuwa na eneo mahususi la kuogolea tofauti na ilivyo sasa hufanya baharini.

Kamishna Idara ya Michezo Zanzibar, Ameir Mohamed Makame amesema sera ya michezo ya Zanzibar ya mwaka 2018 inasema kuendeleza michezo kuogelea ikiwa ni miongoni mwa michezo 41 iliyosajiliwa Zanzibar.

“Hii ni ishara nzuri kuja kuonyesha dalili njema na kuifanya Zanzibar itambulike kwamba inaendesha mchezo huu, watu wajitokeze kushuhudia ugeni huu mkubwa katika sekta ya michezo,” amesema

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Rashid Msaraka amesema hiyo ni fursa kubwa kwa wananchi wa Zanzibar na kwamba usalam utaimarishwa katika maeneo yote atakayotembelea kiongozi huyo.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz