Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais TFF: Fifa imerejesha mpango kutoa fedha

39735 PIC+FIFA Rais TFF: Fifa imerejesha mpango kutoa fedha

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha.Rais wa TFF, Wallace Karia amesema Shirikisho la kimataifa (Fifa) limewarejesha kwenye mpango wa kupewa fedha za miradi ya maendeleo Kalia ametoa kauli hiyo Leo katika mkutano mkuu wa TFF unaondelea kwenye ukumbi wa IACC, Arusha. Karia amesema Fifa imeridhia kuirejeshea Tanzania fedha za miradi ya maendeleo baada ya kuzizuia kwa muda mrefu. Awali kabla ya hotuba ya Karia, Nje ya ukumbi wa mkutano, Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau aliiambia Mcl Digital kuwa, wanatarajia kupata Dola 5,000,000 kutoka Fifa. "Fedha za awali zilikuwa Dola 3,000,000 hivyo sasa wanatupa dola 2 milioni," alisema Kidau. Katika hotuba ya Rais, Karia alisema fedha hizo zitaelekezwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo kuboresha kituo cha Karume

Chanzo: mwananchi.co.tz