Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Mwinyi ahudhuria sherehe uzinduzi wa Olimpiki ya Dunia

Rais Mwinyi Ahudhuria Sherehe Uzinduzi Wa Olimpiki Ya Dunia Rais Mwinyi ahudhuria sherehe uzinduzi wa Olimpiki ya Dunia

Sun, 18 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi amehudhuria sherehe za ufunguzi wa Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu mwaka 2023 katika Uwanja wa Olimpia Jijini Berlin nchini Ujerumani Juni 17, 2023.

Rais Dk. Mwinyi katika msafara wake ameambatana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Balozi Dk.Pindi Chana, Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Dk.Abdallah Saleh Possi.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoshiriki katika michezo hiyo ikitafuta medali kwenye mpira wa wavu na riadha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live