Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raha ya Niyonzima Yanga

14708 Niyonzima+pic TanzaniaWeb

Thu, 30 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigali. Kiungo nguli wa Simba, Haruna Niyonzima ametua nchini hapa na jana alizishuhudia timu zake za zamani zikipambana katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Rwanda, amekuja kujiunga na timu ya Taifa ya Rwanda.

Niyonzima aliwahi kuzitumikia kwa nyakati tofauti Rayon Sports mwaka 2007 kabla ya kutimkia APR alipocheza kwa misimu minne kabla ya kujiunga na Yanga.

Mchezaji huyo aliwasili kwenye Uwanja wa Nyamirambo uliotumika kwa mchezo huo ambao Rayon Sports ilishinda bao 1-0.

Kiungo huyo aliwasili Rwanda juzi akitokea Dar es Salaam kujiunga na timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’.

Licha ya kutoonekana katika klabu ya Simba, Niyonzima ni mchezaji mwenye jina kubwa nchini Rwanda.

Makocha nchini hapa wamekuwa wakimpa umuhimu katika kikosi cha Rwanda kutokana na uzoefu wake.

Chanzo: mwananchi.co.tz