Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rage awapa ujanja Yanga

Rage  Data Rage awapa ujanja Yanga

Mon, 5 Jul 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MWENYEKITI wa zamani wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amewashauri Yanga kuiga mambo mazuri wanayoyafanya wao ili kuwa bora zaidi.

Rage alisema watani zao hao wasiogope kuiga mema kisa ni watani bali waige kwa manufaa ya soka la Tanzania.

Alisema Simba imekuwa bingwa mara tatu mfululizo baada ya kubaini upungufu wao na kuufanyia kazi hivyo Yanga wasione shida kufuata nyayo hizo zitakazowafanya wazidi kuwa bora zaidi.

“Simba ni bora sana kwa sasa hakuna wa kupinga katika hilo, na ili Simba iwe imara inahitajika Yanga imara pia, hivyo wasiogope kuiga kile ambacho Simba wamekifanya kufikia mafanikio hayo,” alisema Rage.

Alisema hatua waliyoianza ya mabadiliko ya kiuendeshaji anawapongeza kwa kuwa soka la sasa linahitaji pesa na sio maneno.

“Uwekezaji ni muhimu sana kwa sasa, nawapongeza kwa hatua waliyoianza kuelekea kwenye mabadiliko hayo kama ambavyo Simba wamefanya.

“Lakini nawasisitiza mwakani tuna uwakilishi wa timu nne, sasa wale ambao wataingia katika uwakilishi huo wajitahidi kufanya usajili mzuri utakaoleta ushindani zaidi.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz