Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rafael Nadal atwaa ubingwa wa Monte Carlo Masters 2018

6942 I TZW

Mon, 23 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Mchezaji tennis, Rafael Nadal amefanikiwa kumfunga Mjapani, Kei Nishikori  kwa seti ya moja kwa moja kwenye mashindano ya Monte Carlo Masters na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo hapo jana siku ya Jumapili.



Nadal amelinda heshima ya kuwa nafasi yake ya kwanza kwenye ubora wa viwango vya mchezo huo dunia baada ya ushindi wa 6-3 6-2  dhidi ya Kei Nishikori.

Kwa ushindi huo utamfanya Mhispania huyo, Nadal kuendelea kusalia katika nafasi yake ya kwanza kwenye viwango vya ubora wa mchezo wa tennis dunia huku mpinzani wake Roger Federer atapaswa kusubiri kuipata nafasi hiyo endapo Nadal atashindwa kwenye michuano ya Monaco.

Mara baada ya kutwaa taji hilo, Rafael Nadal anajiandaa kwaajili ya mashindano ya Ufaransa (French Open).

 

Chanzo: bongo5.com