TIMU za Ligi Kuu Bara zinaendelea kujiimalisha kwa kufanya usajili katika kipindi hiki cha dirisha dogo ambalo litafungwa Januari 15, mwakani huku Yanga wao wakionesha makali katika kipindi hiki kwa kufanya usajili wa wachezaji kadhaa. Uongozi wa Yanga katika kuhakikisha wanakuwa na kikosi imara katika mzunguko wa pili rada zao zimenasa kwa straika wa Gor Mahia ya Ligi Kuu ya Kenya Mghana Gislan Yikpe, ambaye amekuwa mchezaji wa kutumainiwa katika kikosi hiko. Yanga wanamtaka Yikpe, ili kuja kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ambayo katika mzunguko wa kwanza ilikuwa ikibebwa na mshambuliaji Mkongomani David Molinga ambaye mpaka sasa ameifungia timu hiyo mabao manne. Ukimuondoa Molinga ambaye ndio kinara wa kufunga katika kikosi hiko cha Yanga washambuliaji wengine Juma Balinya, Sadney Urikhob na Maybin Kalengo walionekana kushindwa kufanya vizuri na mpaka uongozi wa timu hiyo wakaamua kuacfhana nao. Yanga kama watafanikiwa kumpata Yikpe atakuwa mshambuliaji wa pili waliomsajili katika dirisha dogo ili kuja kuongeza nguvu katika timu hiyo baada ya kumalizana na Ditram Nchimbi, kutokea Polisi Tanzania ambapo alikuiwa katika timu hiyo kwa mkopo.