Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RT yafunguka ishu kambi ya Olimpiki

Michezo Olimpikiiiiiii RT yafunguka ishu kambi ya Olimpiki

Mon, 10 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya ukimya wa muda mrefu kuhusu lini timu ya taifa ya Riadha itaingia kambini kuanza maandalizi ya mashindano ya Olimpiki ambazo zitafanyika Julai jijini Paris Ufaransa hatimaye Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) limevunja ukimya na kusema kambi hiyo itaanza rasmi mapema wiki inayoanza kesho.

Tanzania itawakilishwa na wanaridha wanne pekee wanaokimbia mbio ndefu kilometa 42, Alphonce Simbu, Gabriel Geay, Magdalena Shauri na Jackline Sakilu.

Simbu alifuzu kupitia Shanghai Marathon China akitumia muda wa 2:05:39, huku Jackline Sakilu akifuzu kupitia mbio hizo kwa muda wa 2:26:50, mbio zilifanyika Novemba 26, 2023.

Magdalena yeye alipenya kupitia Berlin Marathon zilizofanyika Ujerumani Septemba 24, 2023 akitumia 2:18:41 huku Geay akitokea Valencia Marathon zilizofanyika Hispania Desemba 2, 2023 kwa 2:04:33.

Wanariadha Andrew Rhobi anayekimbia mita 1500, John Wele mita 5000, Failuna Abdi, ,Josephat Gisemo, Faraja Lazaro na Aloyce Simbu wanaokimbia mbio ndefu wao walishindwa kufuzu.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la RT, Jackson Ndaweka alisema kambi hiyo ambayo itaanza mapema wiki hii katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine tawi la Arusha ambayo lipo Olmotonyi Ngaramtoni itakuwa chini ya makocha wawili.

Makocha hao ni Michael Washa wa Jeshi la Magereza na Antony Mwingereza kutoka Jeshi la Wananchi (JWTZ) ,ambaye wanariadha watatu wamefuzu kushiriki Olimpiki, Simbu, Jackline na Magdalena.

“Tumechelewa kuingia kambini kwa sababu wanaridha wetu walikuwa na mashindano mbalimbali ya Kimataifa hivyo isingekuwa vyema baadhi kuanza huku wengine hawapo”

“Wachezaji wetu wote wapo kwenye hali nzuri ya kimashindano kwani wana viwango bora na wana uwezo wa kucheza chini ya muda ambayo itawafanya kurudi na medali,” alisema Ndaweka.

Aliongeza licha ya kwamba Olimpiki za 2024 zitakuwa na ushindani mkubwa sana kwani wanariadha wengi wenye ubora kwa sasa watashiriki.

Pia kutolewa zawadi za fedha kwa mara ya kwanza kwa washindi ambao watapata medali kwa upande wa Riadha ila wana matumaini makubwa na viijana wao katika kwenda kupambania medali zingine baada ya kupita miaka 44.

Tanzania ilimiliki medali mbili za fedha katika mashindano hayo kwa mbio za mita 1500 na 3000 Olimpiki za Moscow, Urusi mwaka 1980 zilizotwaliwa na Suleiman Nyambui aliyeshika nafasi ya pili katika mbio za Mita 5000 na ile ya Filbert Bayi katika mbio za Mita 3000.

Chanzo: Mwanaspoti