Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RIPOTI: Kampuni ya Nike yavujisha taarifa za usajili wa Coutinho kwenda Barcelona

868 DSVeLEcWAAI114H TZW

Mon, 1 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Kampuni pendwa ya vifaa vya michezo duniani ya Nike kupitia tovuti yake imevujisha taarifa za usajili wa mshambuliaji wa Liverpool, Mbrazili Philippe Coutinho kwenda Barcelona kwa kuweka jezi yake kwenye ukurasa wa klabu ya Barcelona ndani ya tovuti hiyo.

Nike jana waliweka picha ya jezi ya Barcelona ya msimu huu yenye jina la Coutinho, huku wakiambatanisha na ujumbe unaoonyesha kuwa nyota huyo tayari ameshasaini mkataba na Barcelona msimu huu 2017/18 na kuandika ujumbe uliosomeka”Philippe Coutinho yuko tayari kuipamba Camp Nou”.

Hata hivyo baada ya masaa matatu kupita, Nike walifuta link hiyo bila kutoa sababu zozote zilizopelekea kuondoa ujumbe huo na mpaka sasa Barcelona haijatangaza chochote juu ya tukio hilo.

Kwa upande mwingine mashabiki wa Liverpool wameishambulia kampuni hiyo kuwa inashinikiza mchezaji wao ahamie Barcelona kwa kuwa hao ndio wadhamini wa klabu hiyo.

Chanzo: bongo5.com