Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makonda kuwa mgeni rasmi mechi ya Simba na Yanga

7168 Tamasha La Usalama 6 TZW

Sun, 29 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtangaza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara ambao utawakutanisha Simba na Yanga Aprili 29, 2018 katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.



Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Afisa habari wa TFF, Cliford Mario Ndimbo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema Mhe. Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu watakaojitokeza kweye uwanja huo kushuhudia mchezo huo namba 178 utakaoanza saa 10 jioni.

Aidha, Cliford amesema mpaka kufikia sasa tayari tiketi za mchezo huo zinaendelea kuuzwa ambapo VIP A ni shilingi 30,000, VIP B na C 20,000 na mzunguko (Jukwaa la rangi ya Chungwa,Kijani na Bluu) 7,000.

Simba wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 59 ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 23.

Chanzo: bongo5.com