Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makonda avalia njuga tiketi Taifa

48975 Pic+makonda

Wed, 27 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Simba ikijiandaa kucheza na TP Mazembe ya DR Congo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametaka umakini katika uuzwaji wa tiketi ili kuepuka madhara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba na TP Mazembe zinatarajiwa kuvaana katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye uwanja huo Aprili 6.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Makonda ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Stars Ishinde, alisema watahakikisha uwanja huo unaingiza idadi ya watu 60,000 wanaostahili na si vinginevyo.

Makonda alisema wamejifunza kupitia mchezo ambao Taifa Stars iliifunga Uganda mabao 3-0 ambapo mamia ya mashabiki walishindwa kuingia uwanjani licha ya kukata tiketi kutokana na msongamano.

Akizungumzia mchezo dhidi ya Uganda, mkuu huyo wa mkoa alisema kamati yake ilijipanga vyema kuhakikisha Taifa Stars inapata ushindi na kufuzu fainali hizo.

Makonda alisema wamejipanga kuweka utaratibu mzuri kwa Watanzania kwenda Misri kuishangilia Taifa Stars.



Chanzo: mwananchi.co.tz