Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Iringa azindua mashindano Kihenzile Cup

WhatsApp Image 2022 10 31 At 3.jpeg RC Iringa azindua mashindano Kihenzile Cup

Mon, 31 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Halima Dendego amezindua mashindano ya Kihenzile Cup&Awards kwenye Mji Mdogo wa Igowole Wilayani Mufindi.

Kwenye uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa amepongeza jitihada za dhati za waandaji na kuahidi kuwaunga mkono kwenye kazi zao na kuanzia kwa kuchangia ununuzi wa vifaa vya Michezo kwenye Jimbo hilo.

Aidha Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg. George Kavenuke amepongeza sana uzinduzi wa Kihenzile Cup & Awards na kuwataka viongozi wengine kuiga jambo hili jema ili kuendelea kudumisha na kukuza sekta ya michezo Nchini.

Akizungumza kwaniaba ya wabunge waliohudhuria shughuli hizo Mbunge wa kundi la Vijana Mhe. Judith Kapinga akiwa sambamba na Wenzake Mhe Lucy Sabu na Mhe. Fred Lowassa walimpongeza Mhe. Kihenzile na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano wa dhati kwenye azma yake ya kuwahudumia watanzania wa Jimbo la Mufindi Kusini.

Mwenyekiti wa Kihenzile Foundation ambaye pia ni Mbunge wa Mufindi Kusini na Mwenyekiti wa Bunge la Tanzania Mhe David Kihenzile amewaeleza Maelfu ya waliohudhuria Shughuli hiyo kwamba uzinduzi huo ni mwanzo wa mambo mengi makubwa yanayaoratibiwa kuanza mwakani.

Mhe. Kihenzile ameeleza kwamba Michezo mbalimbali imezinduliwa ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu (football), mpira wa pete (netball), kukimbiza Kuku, kukimbia kwenye gunia, riadha nk. Mashindano hayo yanatarajiwa kukamilika baada ya Mwezi mmoja na kisha kuanza maandalizi ya KIHENZILE CUP& AWARDS 2023 sambamba na SAMIA MUFINDI CUP&AWARDS 2023 hivyo wapenzi wa Michezo wajiandae kwa Mambo mazuri na makubwa yanayotarajiwa kuanza.

Kihenzile amewashukuru wote waliohudhuria ikiwemo viongozi, wabunge, wananchi, wadau na wachezaji. Aidha ametoa pongezi za dhati kwa waliodhamini mashindano hayo ikiwa ni pamoja na Benki ya CRDB, Kampuni ya Qwihaya, Kampuni ya Vunjabei, Asas Group, Tanzania Redcross Mkoa Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.

Tayari Kihenzile Foundation imetoa Jezi na Mipira kwa vijiji vyote katika jimbo la Mufindi Kusini na kila Kata imepata seti mbili za jezi na mpira kwa mpira wa miguu (football) na kwa upande wa mpira wa pete (netball) kila kata imepata seti moja ya jezi na mpira mmoja ili kuwezesha timu hizo kuweza kushiriki vyema kwenye Michezo hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wadhamini, Leornad Qwihaya, Mkurugenzi wa Kampuni ya Qwihaya, amepongeza sana jitihada hizo za Mbunge huyo na kuahidi kuendelea kuunga Mkono kazi za Foundation hii kila mara ili iweze kufikia malengo yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live