Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Andengenye asema Lake Tanganyika uko tayari kwa Simba v Yanaga

Dimba Pic Data RC Andengenye asema Lake Tanganyika uko tayari kwa Simba v Yanaga

Sun, 25 Jul 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kigoma. Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amesema uwanja wa lake Tanganyika unatarajiwa kuchezwa mechi ya fainali ya kombe la Azam ASFC Julai 25 upo tayari kwa mchezo huo siku ya kesho.

Akizungumza mara baada ya kukagua uwanja huo, Andengenye ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya uwanja huo, amesema uwanja huo unakamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo.

Amesema ulinzi na usalama upo wa kutosha ndani ya uwanja na nje ambapo na hali ya uwanja iko sawa kwaajili ya mashabiki wa soka na wachezaji.

Katibu wa CCM mkoa, Kajoro Vyahoroka amesema watautunza uwanja huo kwa mechi zijazo kwani wametumia gharama kubwa na hauwezi kubaki kama ulivyokuwa baada ya mashindano hayo.

Amesema wataendea kurekebisha uwanja huo na kuutunza hadi uwe na hadhi ya kucheza mechi za kimataifa na sio kila mchezo ukachezwe Dar es Salaam.

"Baada ya mchezo wa kesho, tutaendelea kurekebisha uwanja wetu na kuutunza ili michezo mikubwa ichezwe hapa kwetu mfano mchezo wa timu yetu ya Taifa na Burundi haina haja kupelekwa mbali inaweza pia kuchezwa hapa kwetu kwasababu uwanja tunao,"amesema Katibu Vyahoroka.

Mbunge wa jimbo la Kigoma mjini, Kilumbe Ng'enda amesema mara baada ya mchezo huo wataanza mashindano ya kombe la mbunge wa Kigoma mjini na kuendeleza timu za mkoa huo kuhakikisha wanafika ligi kuu.

Mapema asubuhi ya leo  timu ya simba ilifika katika viwanja vya Lake Tanganyika kwaajili kukagua uwanja na kocha wa simba Didier Gomes da Rosa na nahodha msaidizi wa timu hiyo Mohammed Hussein kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu maandalizi ya mchezo wa kesho huku timu ya Yanga kushindwa kufika na kuzungumzia maandalizi ya mchezo kama ilivyotaratibu.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz