Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pyramids watua, wawataja Tshishimbi, Balinya

81757 Pyramid+pic Pyramids watua, wawataja Tshishimbi, Balinya

Sat, 26 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Wapinzani wa Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Pyramids wametua leo jijini Mwanza huku Kocha wake Mkuu, Sebastien Desabre akisema anawafahamu vizuri Yanga hususani nyota wake Papy Tshishimbi na Juma Balinya. Akizungumza baada ya kuwasili Kocha huyo,amesema wamekuja kushindana na kusaka ushindi na anaamini mchezo hautakuwa rahisi. "Nawajua Yanga vizuri wakiwamo wachezaji wake kama yule Nahodha (Tshishimbi) na Balinya na ninawajua ni wazuri na mechi itakuwa ngumu ila tunataka ushindi" alisema Sebastien . Katika hali ya kushangaza mmoja wa wachezaji wa Pyramids ambaye mashabiki walimfananisha na Nyota wa Liverpool, Mohammed Salah alifanya kituko kwa kuwarushia chupa ya maji jambo lililofanya mashabiki hao kuanza kushangilia. Kesho timu hiyo inatarajiwa kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ambako ndiko kutachezwa mechi yao dhidi ya Yanga, siku ya Jumapili.

Chanzo: mwananchi.co.tz