Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pwani mabingwa wapya riadha taifa

80b0a3e2054a6842da051ab3796d3346 Pwani mabingwa wapya riadha taifa

Mon, 14 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKOA wa Pwani ndio bingwa mpya wa mashindano ya taifa ya riadha yaliyomalizika jana kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam baada ya kuishinda mikoa mingine 28 iliyoshiriki.

Pwani ambayo inafundishwa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania iliyotwaa medali mbili katika Michezo ya Olimpiki ya Moscow, Urusi Mmarekani Ron Davis, ilistahili ushindi huo wa jumla, baada ya kufanya vizuri katika michezo mingi.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi, aliyetangaza matokeo hayo, mkoa huo ulijinyakulia medali sita za dhahabu, tisa za fedha nane za shaba, ikifuatiwa na Arusha ilitwaa medali tano za dhahabu, saba za fedha na nne za shaba, huku Kusini Unguja ikipata medali tatu za dhahabu.

Mabingwa waliopita wa mashindano hayo yaliyofanyika mara ya mwisho mwaka 2015, Mjini Magharibi, mwaka huu wameshika nafasi ya nne baada ya kupata medali mbili za dhahabu, moja ya fedha na tano za shaba.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe, aliipongeza riadha kwa kuliletea sifa kubwa nchi kwa wachezaji wake kuwahi kufanya vizuri kimataifa kuliko michezo mingine yoyote.

Alisema kuwa mashindano hayo yalisheheni wanariadha wenye vipaji lukuki na kuwa anaamini TOC imeviona na vinatakiwa kuvitunza ili viendelea kufanya vizuri.

Alisema kwa sasa watu wa riadha wanatakiwa kuandaa kazi data na kuwa katika michezo kuna changamoto kubwa ya nidhamu, lakini katika mashindano hayo kumekuwa na nidhamu ya hali ya juu na kutaka iendelezwe.

Aliwataka wanariadha kuendelea kufanya mazoezi na sio kusubiri hadi yanapofanyika mashindano ya taifa. Aliwawataka viongozi na wachezaji kuhakikisha mashindano yajayo yanakuwa na watazamaji wengi.

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo, Alex Mkenyenge, aliwataka viongizi wa mikoa kuwawezesha wachezaji kwenda kushiriki mashindano kama hayo ya taifa badala ya kulalamika kuwa kuna wachezaji wanachaguliwa kutoka baadhi ya mikoa tu.

Chanzo: habarileo.co.tz