Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prisons wao ni mkoa kwa mkoa tu

70678 Prisons+pic

Sat, 10 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

BAADA ya Tanzania Prisons, kumaliza ziara yake Mwanza ambako wamecheza mechi nne, ikishinda mbili na kufungwa mbili, sasa inaelekea Kahama ambako wataendelea kujipima ubavu na timu mbalimbali.

Katibu wa timu hiyo, Ajabu Kifukwe amasema kikosi chao kipo vizuri, wakiamini kwamba ziara wanazofanya zitawapa matunda wakati wa ligi kuu Bara.

Prisons imeshinda dhidi ya Gwambina bao 1-0 (mfungaji ni Ismaili Aziz), Singida United bao 4-1, yakifungwa na Salum Kimenya, Ismaili Aziz, Nurdin Chona na Clephace Anthony Mkandala, lakini wamefungwa na Alliance kwa bao 2-0 na wamefungwa na Mbao2-1.

Katibu huyo ameweka wazi kwamba watakwenda kucheza na Kagera Sugar na Kahama Kombaini, huko mkoan Kahama, akidai baada ya hapo watajua mwelekeo mwingine.

"Tunahitaji kukiandaa kikosi chenye ushindani, baada ya msimu ulioisha kutumia muda mwingi kujinusuru na kushuka daraja, ligi itakuwa ngumu lakini tunahitaji kuwa washindani ambao watakuwa mwiba dhidi ya wale ambao tutacheza nao," amesema na kuongeza;

"Pia malengo yetu ni kuhakikisha tunamaliza nafasi nne za juu ndio mana tupo bega kwa bega na benchi la ufundi kuhakikisha linapata mahitaji yote muhimu ili maandalizi yao yasiwe na dosari," amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz