Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prince Dube aahidi makubwa dhidi ya Rhino Rangers

DUBE Prince Dube aahidi makubwa dhidi ya Rhino Rangers

Wed, 26 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Mshambuliaji hatari wa klabu ya Azam, Prince Dube amesema kuelekea kwenye mchezo wake wa  leo saa 10:00 jioni Mei 26, 2021 wa robo fainali ya kombe la ASFC dhidi ya Rhino Rangers watawapa mashabiki wa Azam kile wanachostahili baada ya mashabiki hao kujitoa sana kwao.

Submitted by George David on Jumatano , 26th Mei , 2021 Mshambuliaji wa Azam, Prince Dube akishangilia bado baada ya kuifunga Yanga miezi miwili iliyopita.

Dube amesema “Ni jambo linalohusu hulka na kwenda pale kupambana kwa ajili ya nembo ya timu, kupambana kwa ajili ya Azam”.

“Unajua mashabiki wetu wamekuwa wakituunga mkono sana katika kipindi kizuri na kibaya, sasa ni wakati wetu kuwalipa kile ambacho wamekuwa wakikitoa kwetu sisi wachezaji”.

Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mahusiano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabiti 'Zaka Zakazi' amesema wachezaji wote wa wanalamba lamba hao wapo fiti kuwavaa Rhino Rangers ya mkoani Tabora anaamini ubora wa kikosi hicho kitawafanya waibuke kidedeana kutinga nusu fainal

Mshindi wa mchezo wa Azam dhidi ya Rhino Rangers kwenye dimba la CCM Kambarage mkoani Shinyanga atacheza na mshindi wa mchezo kati ya Simba na Dodoma Jiji huku Yanga ambaye jioni ya jana aliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mwadui watacheza na Biashara United Mara.

Chanzo: eatv.tv