Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Poulsen atoa sababu Stars kuishika DR Congo

Kochaa Poulsen atoa sababu Stars kuishika DR Congo

Sat, 4 Sep 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akizungumza juzi, baada ya kumalizika kwa mechi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar mwakani, kocha huyo raia wa Denmark alisema ameridhishwa na sare iliyopatikana, kwa sababu walicheza na timu ngumu yenye wachezaji wakubwa.

"Ilikuwa mechi ngumu kucheza ugenini na timu ya DR Congo, timu kubwa kwenye viwango vya soka. Ilikuwa na wachezaji wakubwa waliocheza soka la kulipwa Ulaya na sehemu zingine nje ya nchi yao, mwanzo walionekana kucheza kwa kutudharau wakidhani Tanzania haiwezi kucheza kama ilivyocheza. Sisi tuliwaheshimu, lakini wao walicheza kwa dharau, nadhani baadaye walipoona mambo yanazidi kuwa magumu walibadilika," alisema kocha huyo.

Naye golikipa namba moja wa Stars, Aishi Manula alisema mechi ilikuwa ngumu kutokana na mazingira ya kucheza ugenini.

"Tulikuwa tunacheza na wachezaji wakubwa, lakini ukitaka na wewe kuwa mkubwa, lazima ucheze mechi kubwa na wachezaji wakubwa, tunashukuru kupata pointi moja ugenini," alisema.

Kwenye mechi hiyo ya Kundi J, iliyochezwa mjini Lubumbashi kwenye uwanja unaomilikiwa na klabu ya TP Mazembe, wenyeji walianza kupata bao dakika ya 23 likifungwa na Dieudinne Mbokani, Simon Msuva akiisawazishia Stars dakika ya 35.

Stars itacheza mechi nyingine nyumbani dhidi ya Madagascar Jumanne ijayo, ambayo ilichapwa bao 1-0 nyumbani dhidi ya Benin.

Chanzo: ippmedia.com