Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Poulsen ateua 20 kuunda U-23

76be3dcabdc631a63de59b9b0aece406 Poulsen ateua 20 kuunda U-23

Sat, 17 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23, Kim Poulsen, ameita kikosi cha wachezaji 20 kitakachoingia kambini Julai 19 mwaka huu kujiandaa na michuano ya Cecafa Chalenji nchini Ethiopia.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuhusisha nyota wenye umri zaidi ya miaka 23 ambao wanaruhusiwa kujumuishwa ambao ni Yusuph Mhilu, Reliant Lusajo na Sospeter Israel, timu itaingia kambini siku moja baada ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kutamatika Julai Jumapili.

Akizungumza leo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu, TFF, Dar es Salaam, Poulsen, alisema kuwa katika michuano hiyo, Tanzania imepangwa na mataifa ya Uganda na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hivyo watakuwa na michezo migumu mchezo wa kwanza wanatarajiwa kucheza Julai 22.

“Kikosi hiki kiko kwenye mstari wa mwisho kinajengwa kwaajili ya timu ya taifa ya Tanzania ya kesho,katika kikosi hiki hakuna mchezaji atakayekuja kutoka nje ya Tanzania isipokuwa Nickson Kibabage ambaye yupo hapa hapa nchini,” alisema Poulsen.

Kikosi hicho kinaundwa na walinda mlango Metacha Mnata (Yanga), Daniel Mgore (Biashara United), Wilbol Maseke (Azam FC), mabeki ni Paschal Msindo (Azam), Abdul Majid Mangalo (Biashara) Israel Mwenda (KMC), Nickson Kibabage (Youssoufia FC), Lusajo Mwaikenda (KMC), Sospeter Israel (Azam) na Oscar Masai (Ihefu).

Viungo ni Lucas Kikoti (Namungo), Joseph Mkele (Mtibwa Sugar) , Rajab Athuman na Meshack Abraham (Gwambina),Yusuph Mhilu (Kagera Sugar) na Abdulrazack Hamza (Mbeya City), washambuliaji ni Reliant Lusajo (Namungo), Erick Mwijage (Kagera Sugar), Andrew Simchimba (Ihefu) na Abdul Suleiman (Coastal Union).

Katika Mashindano hayo Tanzania imetoa mwamuzi mmoja msaidizi Kasim Mpanga, ambaye tayari ameondoka nchini kuelekea nchini Ethiopia kwaajili ya michuano hiyo ya vijana ambayo itashirikisha mataifa tisa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz