Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yaiengua Yanga kileleni

4689f2531b304b7513fcbe28809f10db Polisi yaiengua Yanga kileleni

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

POLISI Tanzania imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuishusha Yanga baada ya kuifunga Ruvu Shooting bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani jana.

Polisi ilisubiri hadi dakika ya 78 kupata bao hilo lililofungwa na Vitalis Mayanga.

Kwa ushindi huo, Polisi imefikisha pointi tisa sawa na Yanga, lakini ikiongoza kwa uwiano mzuri wa mabao. Zote zimecheza mechi tatu.

Ruvu Shooting inabaki na pointi sita katika nafasi ya nne ikiwa imecheza michezo minne, ikishinda miwili na sare mbili.

Mchezo mwingine ulitarajiwa kuchezwa jana usiku ni kati ya Dodoma Jiji na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena Ijumaa ya wiki hii, ambapo Mbeya Kwanza itacheza dhidi ya Biashara, Yanga na Azam FC Jumamosi na Simba dhidi ya Coastal Union itachezwa Jumapili.

Chanzo: www.habarileo.co.tz