Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wasimamisha mkutano wa Mzee Kilomoni

68236 Kilomon+pic

Thu, 25 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkutano wa Hamis Kilomoni uliokuwa unaendeleka nyumbani kwake Kinondoni umesimamishwa na Polisi Kanda ya Kinondoni.

Polisi hao wamesimamisha mkutano huo wakitaka kufahamu endapo Mzee Kilomoni amepata kibali cha kufanya mkutano huo.

Kilomoni amekatishwa kuendelea na mkutano huo mara baada ya kukaribishwa ili aanze kuelezea yale aliyowaitia waandishi wa habari.

Mzee Kilomoni ambaye alikuwa mdhamini wa Klabu ya Simba inadaiwa alitaka kuelezea juu ya mwenendo klabu hiyo.

Polisi hao wamemchukuwa Mzee Kilomoni kwenda naye kituo cha Polisi kwa ajili ya kwenda kutoa maelezo kìtuo cha polisi Oysterbay.

"Wao wameniambia nimekatazwa kwamba lazima nikaombe kibali cha kufanya mkutano," alisema Kilomoni

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz