Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tanzania yaikumbuka ligi

POLISI TIMU Polisi Tanzania yaikumbuka ligi

Sat, 30 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA Mkuu wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amesema kikosi chake kimeimarika na kiko tayari kushuka dimbani kumalizia mechi za Ligi Kuu Bara zilizobakia.

Malale aliliambia gazeti hili wachezaji wake 26 wameshaingia kambini na wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu katika kila mechi watakayocheza.

Malale alisema kikosi chake kina wakosa nyota watatu tu, lakini uongozi wa timu hiyo una taarifa za wachezaji hao ambao hawajaripoti kambini.

" Kabla ya kuanza mazoezi tulilazimika kuwapima afya zao wachezaji wote, ikiwamo uzito pamoja na joto, tunashukuru tumekuta wako sawa. Pia tumweweka utaratibu wa kunawa mikono kabla na baada ya kumaliza mazoezi kwa kutumia vitakasa mikono ili kujikinga na corona," alisema Malale.

Aliongeza kwa sasa timu yake inasubiri ratiba kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), na wanaamini shirikisho hilo litatoa ratiba rafiki kwa klabu zote kwa kuzingatia muda uliobakia.

Naye Msemaji wa timu hiyo, Frank Lukwaro alisema wachezaji ambao hawajaripoti mpaka sasa wana matatizo ya kifamilia.

"Wachezaji ambao hawajaungana na wenzao wametoa taarifa, wana sababu za msingi za kuchelewa, tumewapa ruhusa maalumu lakini tunawatarajia hivi karibuni," alisema Lukwaro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live