Mchezaji wa zamani wa klabu ya soka ya Manchester United, Roy Keane, amemjia juu Paul Pogba kwa kudai kuwa uchezaji wake ndani ya timu ni kama mtoto wa shule.
Roy Kean akiongeza na kituo cha ITV
Keane amesema hayokupitia kituo cha runinga cha ITV cha Uingereza baada ya Man United kutolewa katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya usiku wa juzi na Sevilla kwa mabao 2-1 katika uwanja wa Old Traford.
“Pogba ni tatizo kubwa na kama hawezi kupata kuanziakwenye kikosi cha kwanza basi yuko katika shida. Unatarajia wachezaji wakubwa kuja na kubadili mchezo. Aliingia usiku wa jana na hakufanya chochote. Tuliona kwenye goli la kwanza, reaction yake ilikuwa kama mtoto wa shule,’ amesema Keane.
“Sababu wewe ni sehemu ya timu, wakati mwenzio kwenye timu anafanya kosa, unasawazisha. Hakuna hata mmoja anamsaidia mwengine na hawachezi kama wapo timu kubwa ya United ambapo unapaswa kuchimba matokeo hata wakati wa usiku. Wanacheza kama watu binafsi na hawaonekani wana uwezo wa kufanya hivyo,” ameongeza.