Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pluijm nd’o basi tena! Kutimka nchini leo

44844 PIC+PLUI Pluijm nd’o basi tena! Kutimka nchini leo

Tue, 5 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

BAADA ya kutumika nchini kwa miaka mitano, kocha wa Kiholanzi Hans van der Pluijm  anatarajia kuaondoka leo jioni  kurejea kwake Ghana kwa ajili ya kukaa na famili yake.

Pluijm ambaye hivi karibuni kibarua chake kiliota nyasi Azam na nafasi yake kurithiwa na Meja mstaafu Abdul Mingange akisaidiwa  na Iddi Cheche, aliwahi pia kuzinoa Singida United na Yanga.

Akiwa katika maandalizi ya kuondoka nchini Pluijm alisema kinachoweza kuiangusha Tanzania kufikia kilele cha mafanikio kisoka kama mataigfa ya Afrika Mgharibi ni uvumilivu.

“Nimejifunza vingi Tanzania, upande wangu hili ni moja ya taifa la mpira ila linashida ndogo ndogo ambazo kama zitatatulia linaweza kuwa  moja ya mataifa makubwa kisoka.

“Hakuna kitu kizuri kama kuwa na mipango ya muda mrefu, siku zote matokeo yake huwa ni makubwa, mipango ya muda mfupi inahitajika sehemu ambayo tayario wanamisingi mizuri ya mpira na sio Tanzania,” alisema kocha huyo.

Pluijm alisema miongoni mwa wachezaji ambao atawakumbuka akiwa Ghana ni Mudathir Yahya kutokana na uwezo wake wa kucheza soka la kisasa linalohitaji mtu mwenye ubunifu hasa kwenye eneo la kiungo mkabaji.

Mholanzi  huyo mwenye umri wa miaka 70,  ameacha rekodi nchini ya kutwaa mataji matatu mfululizo  ya Ligi Kuu Tanzania Bara .Alianza kushinda msimu wa 2014/15 kabla ya kutwaa tena 2015/16 na  2016/17.



Chanzo: mwananchi.co.tz