Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pluijm aihofia JKT Tanzania

Sun, 22 Apr 2018 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA wa Singida United, Hans Pluijm amesema JKT ni timu ngumu na hatari, kama wakiidharau wanaweza kushindwa kufika fainali za michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (FA).

Timu hizo zinatarajiwa kukutana kesho kwenye uwanja wa Namfua Singida, katika mchezo wa nusu fainali, akitafutwa mshindi wa kuungana na Mtibwa Sugar kwenye fainali.

Akizungumza na gazeti hili jana, Pluijm alisema mpaka kufikia hatua hiyo JKT si timu ya kubeza kwani watakuwa na kazi kubwa kuwatoa.

“Tusipokuwa makini tunaweza tusifike fainali kwa sababu JKT wako vizuri na siyo timu ya kubeza, tumejipanga kuhakikisha tunapambana kutimiza malengo yetu,” alisema.

Alisema walikuwa kambini tangu Jumanne kwa ajili ya kukiandaa kikosi chake kimchezo, kisaikolijia na kiafya na kwamba wana imani watakwenda kucheza kwa moyo uleule waliotumia kwenye michezo iliyopita.

Tayari wapinzani wao JKT waliwasili mkoani humo wakisubiri mchezo huo huku Kocha wa kikosi hicho, Bakari Shime akipania kuweka rekodi ya kutinga fainali.

Shime alisema ameshawasoma Singida, hivyo watatumia udhaifu wao kwa ajili ya kutengeneza nafasi na kuitumia ipasavyo ili kufikia lengo lao la kucheza fainali na kushinda taji litakalowapa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.

Chanzo: habarileo.co.tz