Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pique akiri Barca kuna matatizo makubwa

Pique Pique akiri Barca kuna matatizo makubwa

Mon, 4 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

GERARD Pique amekubali Barcelona haikuwa bora wakati wakichezea kichapo kutoka kwa Atletico Madrid na amesema hata kama wangecheza kwa saa tatu wasingeweza kufunga bao.

Miamba hao wa Catalunya walikumbana na kipigo cha pili mfululizo kwenye mashindano yote na mchezo wao wa kwanza kwenye LaLiga tangu Mei – wakati walipofungwa mabao 2-0, Jumamosi.

Barca walipiga mashuti mawili tu ya kulenga bao katika dakika zote 90 kwenye mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Wanda Metropolitano.

Memphis Depay, ambaye amekuwa na mashuti mengi ya kulenga bao kwenye LaLiga (13, sawa na Karim Benzema wa Real Madrdi, hakufurukuta kabisa kwenye mchezo huo.

Atletico walikuwa kwenye kiwango bora, wakifunga mabao mawili katika mashuti sita yaliyolenga bao, Luis Suarez alitengeneza bao la kwanza lililofungwa na Thomas Lemar kabla yeye kufunga la pili.

Barca sasa imeruhusu mabao matano bila wao kufunga katika mechi mbili zilizopita, na Pique, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi wakati wakifungwa na Benfica kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya katikati ya wiki, amesema kikosi chao kinahitaji kufanya kazi ya ziada.

"Tulianza vizuri, lakini walifunga mabao mawili yanayofanana," alisema akiiambia Movistar.

"Mambo ni magumu sana kwa upande wetu. Tupo kwenye wakati mgumu na kuna matatizo kadhaa.

"Watu tayari wanajua matatizo yetu. Hata mtu kipofu anaweza kuona nini tunachokikosa. Lakini tutarudi kwenye ubora wetu hivi karibuni.”

Chanzo: ippmedia.com