Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pierre akabidhiwa tiketi ya VIP kwenda AFCON

63483 Piereepic

Wed, 19 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza leo amemkabidhi Mchekeshaji, Peter Molel maarufu kwa jina la Pierre Konki Liquid tiketi ya ndege ya VIP kwenda na kurudi nchini Misri kwa ajili ya kuhamasisha ushangiliaji kwa Taifa Stars.

Taifa Stars inashiriki katika michuano ya Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) ambapo imepangwa kundi C pamoja na timu za Senegal, Algeria na Kenya.

Juni 23 Stars wanatarajiwa kushuka dimbani kucheza dhidi ya Senegal ambapo wabunge 50 wanaokwenda kesho nchini Misri wanaungana na Watanzania wengine kwa ajili ya kuhamasisha na kushangilia timu hiyo.

Akizungumza leo Juni 19 2019, Shonza amesema wamemwita kumkabidhi tiketi hiyo kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

“Leo tumemwita kumkabidhi tiketi ambayo Waziri Mkuu aliahidi kuwa ataitoa kwa ajili ya kumpeleka na kumrudisha ndugu yetu Liquid kwa ajili ya kwenda kuwa mhamasishaji,” amesema.

 “Kwa hiyo sisi kwa niaba ya wizara tunamshukuru Waziri Mkuu lakini kipekee tunawashukuru waliogharamia safari ya Liquid kwenda na kurudi,” amesema.

Pia Soma

Amesema wabunge wamejitokeza kwa wingi kuhakikisha wanaenda kushiriki katika kuhamasisha na kushangilia timu hiyo.

Amewaomba Watanzania kuendelea kuichangia timu hiyo na kwamba kesho kuna harambee jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Ameaomba wadau wa michezo na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuchangia ili ifanye vizuri ikiwa ni sehemu mojawapo ya kutoa hamasa kwa timu hiyo.

“Tunadiriki kusema timu yetu ipo vizuri, na tunaamini imejiandaa na kujipanga vizuri kikubwa ni kwamba tutaendelea kuisapoti kama ambavyo tunafanya lakini kikubwa ni kuichangia ili kuongeza hamasa kwa vijana hawa ili wafanye vizuri zaidi,” amesema.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA), Adrian Nyangamalle alisema Pierre ni msanii anayeshughulika na biashara za mbao anatambulika na mradi wa sanaa za ufundi (TACIP).

Amesema hivyo waliona ni muhimu kusaidia kufanikisha safari hiyo ili ahadi ya Waziri Mkuu ifanikiwe.

”Pierre kule unapoenda ukazidi kuhamasisha ili ile amsha amsha ikaendelee kwa sababu tunajua kuwa mashabiki ni mchezaji wa 12 katika timu yoyote ile, hivyo tunaamini msafara huo utasadia timu yetu kufarijika,” amesema.

Naye Pierre, amewamshukuru wabunge na kumwombea Majaliwa aishi miaka 100 kwa kutamka kuwa atabaki juu kileleni.

“Tunaelekea Misri na tutashinda, tutashinda, tutashinda tutabaki kuwa juu mawinguni..” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz