Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Picha: Ronaldo alivyoandaa party ya kufunga mwaka na familia yake

728 25026265 536629970023465 6657358763755831296 N TZW

Thu, 28 Dec 2017 Chanzo: bongo5.com

Mwaka 2017 umekuwa na mafanikio makubwa kwa Cristiano Ronaldo – Hakuna ubishi kwenye hilo.

Cristiano Ronaldo akiwa na mpenzi wake Georgina Rodriguez

Miongoni mwa mafanikio ambayo amepata mchezaji huyo katika mwaka huu ni pamoja na kupata watoto watatu ambapo wawili ni mapacha, kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara ya tano, tuzo ya mchezaji bora wa Fifa, La Liga, Champions League, Spanish Supercup, European Supercup, na Fifa Club World Cup.

Katika kulitambua hilo Ronaldo ambaye anacheza Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno aliamua kuandaa sherehe ya familia kwa ajili ya kuuaga mwaka kutokana na mafanikio hayo makubwa aliyoyapata.

Cristiano Ronaldo akiwa na familia yake katika sherehe yake ya CR7 Gala

Sherehe hiyo aliipa jina la ‘CR7 Gala’ na ilihudhuriwa na watu wake wa karibu akiwemo mpenzi wake Georgina Rodriguez, mama yake mzazi Dolores Aveiro, dada zake Katia and Elma, na kaka yake Hugo.

Chanzo: bongo5.com