Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Picha: Nike yamtunuku Harry Kane vifaa vipya baada ya hili

2671 48E2705E00000578 5350777 Kane Poses For Pictures With His Tottenham Team Mates After Resc A 10 TZW

Wed, 7 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Uingereza, Harry Kane amekabidhiwa vifaa vipya vya mchezo wa soka na kampuni ya Nike baada ya hapo jana siku ya Jumapili kufikisha jumla ya mabao 100.



Kane alifikisha idadi hiyo ya mabao 100 hapo jana baada ya kufunga bao moja kwa njia ya mkwaju wa penati na kuisaidia timu yake ya Spurs kutoka sare ya 2 – 2 dhidi ya Liverpool huku mshambuliaji huyo akikosa penati kabla ya kufunga goli hilo.



Sasa mchezaji huyo anafikisha idadi ya magoli hayo 100 akiwa ameichezea timu hiyo jumla ya michezo 141.

    

Picha zinazo muonyesha Kane akikabidhiwa baadhi ya zawadi na kusherehekea na wachezaji wenzake baada ya kufikisha idadi ya mabao 100.



Chanzo: bongo5.com