Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pep Guardiola agoma kuingia kandarasi mpya Manchester City

3812 05CC8BB2000003E8 5426541 Image M 70 1519388289550 TZW

Tue, 27 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amegoma kuingia kandarasi mpya mpaka pale atakapo hakikisha anaipatia taji timu hiyo.



Guardiola ambaye alikuwa kocha wa Barcelona amekubali kandarasi mpya aliyopewa na City itakayo mfanya kusalia katika viunga vya Etihad mpaka mwaka 2021 lakini kwa upande wake amenuwia kutomwaga wino hadi atakapo iwezesha timu hiyo kunyakuwa taji.



Mkataba huo wenye thamani ya pauniĀ  milioni 20 kwa mwaka utamfanya kocha huyo kuendelea kukinoa kikosi cha City ilhali ule wa sasa ukitarajiwa kufikia tamati mwishoni mwa msimu.

Mhispania huyo hakuwa na uhakika kama angekuwa zaidi ya miaka mitatu lakini hatimaye anasalia na kuendeleza ‘project’ yake City.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zimesema kuwa, Guardiola anachohitaji ni kuhakikisha anatwaa taji lake la kwanza hapa kabla ya kusaini mkataba mpya na klabu.

Kikosi cha City kitakuwa na kazi kubwa wiki ijayo pale iatakapo kutana na Arsenal siku ya Jumapili katika kupigania taji la Carabao Cup katika dimba la Wembley.

Mmiliki wa klabu hiyo, Sheikh Mansour hana wasiwasi na Guardiola baada ya kukionyeshea dira kikosi cha timu hiyo huku ikiongoza ligi hiyo kwa wastani mzuri.

Chanzo: bongo5.com