Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Penalti 19, Makambo peke yake kakosa

45630 Pic+penat Penalti 19, Makambo peke yake kakosa

Sun, 10 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo ni mchezaji pekee aliyekosa penalti kati ya 19 zilizopigwa hadi sasa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Makambo kinara wa ufungaji wa Yanga alikosa penalti yake katika mchezo dhidi ya Alliance uliochezwa jijini Mwanza na Yanga kushinda bao 1-0 lililofungwa na Amis Tambwe akitengenezewa pasi na Mkongo huyo.

Wakati Makambo akikosa penalti nahodha wake wa zamani beki Kelvin Yondani ndiye mchezaji wa kwanza kufunga penalti msimu huu katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar na kuisaidia Yanga kushinda 2-1.

Penalti ya pili ilifungwa Agosti 27 mwaka jana na kiungo wa Azam FC, Tafadzwa Kutinyu katika ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Ndanda FC.

Mshambuliaji wa zamani wa Mbeya City, Eliud Ambokile ndiye aliyefunga penalti ya mapema zaidi katika dakika ya 10 ya mchezo walioshinda mabao 2-0 dhidi ya Stand United Oktoba Mosi mwaka jana.

Penalti nyingine ilifungwa na Habib Kiyombo wa Singida United katika dakika ya 29 na timu yake kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC. Nyota wa Mbeya City, Idd Seleman aliifunga penalti yake dakika ya 60 na kuisaidia Mbeya City kushindi mabao 4-2 dhidi ya Ruvu Shooting.

Jean Marie Girukwishaka aliifungia Mwadui bao la ushindi kwa penalti ya dakika ya 29, wakichapa Lipuli 1-0. Naye Ramadhani Kapera wa Kagera Sugar aliisawazishia  timu yake kwa penalti wakilazimisha sare bao 1-1 dhidi ya Singida United.

Mshambuliaji Said Dilunga wa Ruvu Shooting alifunga penalti mbili katika mchezo huo na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Stand United. Ramadhani Kapera wa Kagera Sugar alifunga bao la kufutia machozi dakika ya 32 kwa penalti baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga.

Emmanuel Elfadhil wa Tanzania Prisons alifunga penalti dakika ya 45, kabla ya Ajibu kufunga penalti dakika ya 76 Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. Nyota wa zamani wa Azam, Yahya Zayd aliifungia timu yake kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 72 katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stand United.

Jumanne Elfadhil alifunga penalti dakika 60 aliifungia Tanzania Prisons bao la kufutia machozi wakiambulia kipigo cha mabao 5-1 kutoka KMC.

Mshambuliaji Vitalis Mayanga alifunga penalti dakika ya 30, Ndanda FC ikishinda bao 1-0 dhidi ya African Lyon.

Dakika ya 32, Bigirimana Blaise alifunga bao kwa mkwaju penalti katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

Nyota Jumanne El Fadhil alifunga penalti katika dakika ya 90 na kuisaidia Prisons kushinda 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar. Penalti ya mwisho ya Omary Mponda aliifungia Kagera Sugar ikishinda 2-1 dhidi ya Biashara United.



Chanzo: mwananchi.co.tz