Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pawasa awafunda Bocco, Kagere

15731 Pic+pawasa TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Safu ya ushambuliaji Simba imetakiwa kuongeza kasi katika Ligi Kuu Tanzania Bara kama inataka kutetea ubingwa msimu huu.

Akizungumza Dar es Salaama jana, beki wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa, ambaye kwa sasa ni Kocha wa timu ya Taifa ya soka la ufukweni, alisema ameshitushwa na ubutu wa washambuliaji katika mechi mbili za Ligi Kuu.

Pawasa alisema ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Prisons na mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City ilipozikaribisha kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, sio dalili njema kwa mabingwa hao.

Alisema Simba yenye kikosi kipana katika safu ya ushambuliaji ilipaswa kutengeneza nafasi nyingi za mabao, lakini hawajafanya hivyo.

“Simba kama itaendelea na tabia ya kufunga bao moja kama ilivyokuwa dhidi ya Prisons kutakuwa na tatizo, wachezaji wanapaswa kujua mabao yana faida yake,” alisema Pawasa.

Alisema timu hiyo inayosifika kuwa na washambuliaji hodari wenye uwezo wa kufunga inapaswa kufunga idadi kubwa ya mabao na pia isiendelee kumtegemea Kagere pekee.

Wakati Pawasa akisema hayo, Bocco ambaye ni nahodha wa Simba alimtoa hofu akisema wachezaji wote wamejipanga kushinda kila mchezo na kwa sasa wanaendelea vyema na maandalizi chini ya kocha Patrick Aussems.

Simba itashuka uwanjani kuvaana Ndanda ya Mtwara katika mchezo wa Ligi utakaopigwa Septemba 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.

Chanzo: mwananchi.co.tz