Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pawasa aonya vijeba mashindano ya vijana U-17

Pawasa Vijeba Pawasa aonya vijeba mashindano ya vijana U-17

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Boniface Pawasa amewataka viongozi na makocha wa timu 14 zinazoshiriki mashindano ya Vijana U-17 kuzingatia umri sahihi na kuacha udanganyifu ili kulisaidia taifa kutengeneza msingi mzuri na kuzalisha vipaji vitakavyosaidia miaka ijayo.

Pawasa ambaye ni moja ya timu ya ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwenye mashindano hayo yaliyoanza jana Jumatano jijini hapa, ametoa kauli hiyo wakati akiongoza usaili wa wachezaji na droo ya kupanga makundi katika kituo cha Alliance, kabla ya jopo kuchuja bora kwa ajili ya timu za taifa.

Amesema suala la udanganyifu wa umri limekuwa likiligharimu taifa katika soka la vijana, huku akiwataka makocha kuwa na mtazamo chanya wa kulisaidia taifa kwa kuzalisha vijana sahihi na siyo kuangalia kupata ushindi wa muda mfupi.

“Wote mnajua miaka mingi tumekuwa tukipiga mark time tu, tukitaka shortcut kuleta wachezaji waliozidi umri tutakuwa hatuwasaidii hawa wachezaji kwa sababu akifika hatua ya timu ya taifa kuna vipimo vya umri na hicho kipimo ndiyo mchawi wetu,” amesema Pawasa na kuongeza;

“Ilishatutokea wakati fulani timu ya taifa ilikuwa inahitajika kwenye mashindano nje ya nchi siku ya kusafiri wakati tunakamilisha vipimo tukabaki na wachezaji nane tu ikabidi tuite wale tuliowaacha, hivyo tuliingia usumbufu mkubwa. Tusiangalie matokeo tuangalie kuandaa kesho yetu.

Mratibu wa waamuzi katika michuano hiyo Kanali Isalo Chacha, amesema jumla ya waamuzi 16 watachezesha mashindano hayo, huku akizionya timu kutofanya hila za kutaka kuwatumia waamuzi kuwabeba na badala yake zipambane kusaka ushindi kihalali uwanjani.

“Moto wetu sisi ni kumpata bingwa halali hatumtazami mtu usoni na kumbeba tujitahidi kadri tuwezavyo apatikane mshindi halali na siyo kwa nguvu ya pembeni. Hatutaki kusikia kitu kinachoitwa rushwa kila timu ijitahidi kucheza kwa uwezo wake na kushinda kihalali,” amesema Chacha.

Chanzo: Mwanaspoti