Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Parker yupo fiti kumvaa Anthony Joshua wiki hii – Scott

5337 Wbo Heavyweight Champ Joseph Parker Is Good Just Not Good Enough TZW

Mon, 26 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Bingwa wazamani wa uzito wa juu duniani, Malik Scott amesema kuwa Joseph Parker yupo fiti asilimia 100 kupigana na Anthony Joshua wiki hii. 

Anthony Joshua ajigamba kuelekea pambano lake dhidi ya Parker

Scott ambaye ni raia wa Marekani amethibitisha kuwa Parker amefanyiwa upasuaji kabla halijaja dili la kupambana na Joshua na kusema yupo tayari kuwania ubingwa huo wa WBA na IBF huko Cardiff siku ya Jumamosi ya Machi 31.



Malik Scott amerejea tena katika mchezo huo wa masumbwi mwezi Septemba baada ya kumsaidia Parker kutwaa ubingwa wa dunia dhidi ya Hughie Fury.

Joshua awapa neno mashabiki wake kuhusu pambano lake na Joseph Parker

Bondia huyo wazamani yupo upande wa timu ya Mnew Zealande, Joseph Parker huku akiongeza kuwa kwa sasa ngumi yake inauzito mkubwa zaidi tangu kufanyiwa operesheni mwaka uliyopita.

Chanzo: bongo5.com