Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Parasports, mabingwa Kenya kukipiga Dar

Paralysts.jpeg Parasports, mabingwa Kenya kukipiga Dar

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nifuate Foundation kwa kushirikiana na Sauti Parasports Club wameandaa mechi ya kirafiki ya kimataifa, kati ya Sauti Parasports Club na Mombasa Amputee kutoka nchini Kenya itakayopigwa Aprili 28 kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Sauti Parasports, Abdul Ally 'Mashine' aliliambia Mwanaspoti kuwa; "Kumekuwa na mwitikio mdogo, hivyo mechi hii itasaidia kupata uzoefu na maandalizi ya kimataifa na tunaamini kupitia mchezo huu tutaweza kutatua changamoto zetu mbalimbali kama usafiri kwa wachezaji kwa maana ya ule wa ndani na nje, nyumba ya kukaa au kukodi, gari ya wagonjwa jambo ambalo kwa sapoti ya Serikali tunaweza kufanikisha."

Nahodha wa Mombasa Amputee, Albert Kalama alisema maandalizi ni makubwa kwa mchezo huu na kwamba kuanzia jana hadi Aprili 23 watakuwa kambini.

Katibu Mtendaji wa BMT, Neema Msitha aliipongeza Sauti Parasports kwa jitihada ya kuandaa mchezo huo wa kimataifa.

Chanzo: Mwanaspoti