Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Panga Kubwa Lapita Azam

AZAM 1?fit=1080%2C722&ssl=1 Panga Kubwa Lapita Azam

Mon, 19 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Panga Kubwa Lapita Azam July 19, 2021 by Global Publishers



UONGOZI wa Klabu ya Azam, upo kwenye mipango ya kupitisha panga kubwa ndani ya kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya kufanya maboresho ya kushusha nyota wapya na kuachana na baadhi ya waliopo ambao hawakutoa mchango uliostahili.

Azam imepata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao baada ya kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Katika michuano hiyo msimu ujao, Azam itakuwa sambamba na Biashara United iliyo nafasi ya nne kwenye msimamo, huku mabingwa Simba na Yanga wakipata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Msaidizi wa Azam, Vivier Bahati, alisema: “Kwanza tunajivunia sana nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao. Haya ni mafanikio ya malengo yetu kwa msimu huu.

“Kuelekea michuano hiyo, tumejipanga kuhak–ikisha tunafanya vizuri na ni lazima tuandae kikosi kitakachokuwa imara kwa ajili ya kuweka heshima, hivyo tunatarajia kufanya usajili wa maboresho katika maeneo ambayo tunadhani yana mapungufu.“

Katika mpango huo, tutaachana na baadhi ya wachezaji ambao tunadhani hawakuwa na mchango ambao tuliutegemea.”

Share this:TweetWhatsApp Related

Chanzo: globalpublishers.co.tz