Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pambano lililo kosekana bingwa kurudiwa

Wed, 31 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Bondia Gennady Golovkin anatarajia kukutana na mwanamasumbwi Saul ‘Canelo’ Alvarez katika mchezo wa marudiano wa kuwania ubingwa wa dunia uzito wakati Mei 5 mwaka huu.



Pambano hili ambalo la marudiano linatarajiwa kupigwa Las Vegas baada ya lile la kwanza lililofanyika mwezi Septemba na kumalizika kwa sare kugubikwa na utata.

Kazakh Golovkin mwenye umri wa miaka 35, atatetea tena mikanda yake ya WBA, WBC na IBF dhidi ya Mexican Alvarez mwenye umri wa miaka 27.

Golovkin  ambaye amepigana mapambano 38 pasipo kupigwa hata moja amesema kuwa hili ndilo pambano ambalo dunia inahitaji.

Pambano lao la kwanza maamuzi yalitoka kwa Alvarez kupata pointi  118-110 ,na 115-113 kwa Golovkin sare ya tatu ikawa 114-114 jambo ambalo Golovkin aliyaita matokeo hayo kuwa ni mabovu katika mchezo.

Chanzo: bongo5.com