Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pablo awataja Mastaa Watatu Simba

Pablo Train Pablo awataja Mastaa Watatu Simba

Fri, 19 Nov 2021 Chanzo: globalpublishers

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, mapema tu ameonekana kuridhishwa na viwango vya baadhi ya mastaa wa timu hiyo, huku akianza kuwataja watatu aliowaona siku ya kwanza.

Pablo raia wa Hispania, alitangazwa kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Novemba 6, mwaka huu akichukua mikoba ya

Mfaransa, Didier Gomes. Baada ya kutambulishwa, akajiunga rasmi na timu hiyo, Novemba 10.

Kocha huyo ambayealianza kusimamia mazoezi ya timu hiyo Novemba 12, siku moja kabla ya hapo alishuhudia Taifa Stars kikicheza mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya DR Congo.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, ulimalizika kwa DR Congo kushinda 3-0, ambapo Pablo

alikuwa jukwaani, lengo ni kuwaona nyota wa Simba.

Baada ya mchezo huo, Pablo alizungumzia viwango vya wachezaji wake wa Simba akiwasifu

Aishi Manula, Shomari Kapombe na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.

“Aishi aliokoa mabao akiwa anatazamana na mpigaji, pia alipangua michomo kadhaa, ni kipa mzuri, Shomari na Mohammed nimewaona ni wazuri kwenye kukaba na kushambulia pia.

Nimefurahi kuwaona,” alisema kocha huyo ambaye alikuwa msaidizi kunako kikosi cha Real Madrid mwaka 2018.

Katika mechi hiyo, wachezaji wa Simba walioanza kikosi cha Taifa Stars ni Manula, Kapombe,

Tshabalala, Kennedy Juma na Kibu Denis, huku John Bocco, Erasto Nyoni na Mzamiru Yassin wakiingia

kipindi cha pili.

Mzamiru aliingia dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Novatus Dismas, Nyoni alichukua nafasi ya Kennedy dakika ya 58, huku Bocco akiingia badala ya Kibu dakika ya 59. Kapombe alitoka dakika ya 71 kumpisha Kibwana

Shomari, wakati Manula na Tshabalala wakimaliza dakika zote tisini.

Wakati Pablo akiwataja mastaa hao watatu, taarifa kutoka kwa mtu mmoja wa benchi la ufundi la Simba, zinasema kuna baadhi ya wachezaji wanaweza wasimalize msimu huu wakiwa kikosini hapo.

Hiyo ni kufuatia kocha huyo kutoridhishwa na uwezo wao baada ya kuwasimamia mazoezini kwa takribani siku sita.

“Baada ya kuangalia mechi ya kirafiki dhidi ya Cambiaso (ilichezwa Novemba 13, mwaka huu na kumalizika kwa sare ya 2-2), kocha hakufurahishwa na viwango vya baadhi ya wachezaji waliocheza mechi hiyo, hivyo kuna uwezekano mkubwa kwenye dirisha dogo wakatolewa kwa mkopo au kuuzwa kabisa,” alisema mtoa taarifa huyo.

Baadhi ya wachezaji wanaotajwa kuwa kwenye orodha ya hao wanaoweza kuondolewa ni Jeremiah

Kisubi na Abdulswamad Kassim.

Chanzo: globalpublishers