Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pablo aomba wiki tatu kuiweka sawa Simba

Pablo Train Pablo aomba wiki tatu kuiweka sawa Simba

Tue, 16 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco ameomba wiki tatu ili kikosi chake kiweze kucheza kwa ushindani katika mashindano yote yajayo.

Simba ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la FA na wanatarajia kucheza dhidi ya Red Arrows ya Zambia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Pablo alisema tangu aanze majukumu ya kuifundisha timu hiyo ameshuhudia vipaji vya hali ya juu kwa wachezaji wake.

"Nafurahi kuona kazi yangu haitakuwa ngumu sana kutokana na uwezo walionao wachezaji niliowakuta hapa, bado nasubiri wale waliopo timu ya taifa nadhani wiki tatu zitatosha kutufanya kuwa bora," alisema Pablo.

Kocha huyo raia wa Hispania alisema kitu kikubwa ambacho anakifanya kwenye mazoezi ni kujenga muunganiko utakaofanya timu hiyo icheze kwa uelewano.

Alisema anajua falsafa ya Simba ni kupiga pasi nyingi, na hilo anataka kuliongezea vitu ili liweze kunoga na kuwachanganya wapinzani wao kitu ambacho kitawasaidia kupata ushindi kirahisi.

Aidha, kocha huyo alisema kuelekea mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows wanaendelea na maandalizi, huku akiwasoma wapinzani wao ili kujua mbinu zao.

Pablo amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akichukua mikoba ya Mfaransa, Didier Gomes ambaye aliamua kuachia ngazi baada ya timu hiyo kushindwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa na Galaxy

Chanzo: www.tanzaniaweb.live