Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pablo: Tuko tayari kwa pointi tatu, nitafurahi nikiwafunga Barcelona

Pablo 5 Pablo: Tuko tayari kwa pointi tatu, nitafurahi nikiwafunga Barcelona

Thu, 18 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco amesema Kwa namna alivyoitazama Ruvu Shooting ikicheza dhidi ya Yanga imetosha kueleza ubora wa timu na kikosi walichonacho hivyo hatokwenda kizembe lakini yuko tayari kwa ushindi wa kwanza kwenye Ligi.

Akizungumza katika kikao cha maandalizi ya mchezo huo na waandishi wa habari leo katika hotel ya Lake jijini Mwanza, Pablo amesema anafahamu Ruvu wana motisha kubwa na wanauhitaji mchezo huo lakini kikosi chake kimejiandaa kushinda kesho.

Pablo amesema kama Ruvu inaitwa Barcelona ya Bongo basi atafurahia kuifunga kesho kwa sababu yeye ni shabiki wa muda mrefu wa Real Madrid.

"Ruvu shooting ni timu nzuri yenye ushindani tuliwatazama dhidi ya Yanga lakini tuko tayari kwa kesho kutoa mchezo mzuri na kupata pointi tatu muhimu," amesema Pablo.

"Wachezaji walinikaribisha vizuri wananisikiliza na wanaonyesha  bidii mazoezini hii inatia moyo kwa sababu Simba ni moja ya timu kubwa Afrika  yenye wachezaji wengi wazuri," amesema.

Amesema pamoja na ugeni wake lakini atahakikisha anawapatia furaha mashabiki wa Simba huku akiamini timu hiyo itaimarika kadri siku zinavyokwenda na kupata kikosi cha kwanza

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz