Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pablo: Ligi bado mbichi

446722c2e5803e0953041643c9a11c1b.jpeg Pablo: Ligi bado mbichi

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: Habarileo

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco amesema licha ya afya za wachezaji wake kutetereka hivi karibuni, lengo la kutetea ubingwa wao bado lipo palepale na kwamba ligi bado mbichi.

Simba inayoshikilia rekodi ya kutwaa taji la Ligi Kuu kwa misimu minne mfululizo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ikikusanya pointi 18 katika mechi nane ilizocheza mpaka sasa.

Akizungumza na gazeti hili jana, kocha huyo raia wa Hispania, alisema haoni sababu ya kuwapa presha wachezaji wake kwa ajili ya utofauti wa pointi tano ambazo wameachwa na wapinzani wao Yanga wakati ligi bado mbichi.

“Afya ni jambo la msingi ndio linaloleta matokeo mazuri kwa hiyo siwezi kuwatia presha wachezaji wangu kwasababu ya kuwa nyuma kwa pointi tano, naamini vijana wangu watafanya kazi na mwisho wa msimu tutakuwa mabingwa kama ambavyo tumekusudia,” alisema Franco.

Kocha huyo mwenye rekodi yakutopoteza hata mchezo mmoja wa Ligi Kuu tangu ajiunge na miamba hiyo miezi miwili iliyopita, amefananisha mwenendo wa ligi kuwa ni sawa na mbio za marathoni hivyo hata kama yeye timu yake ingekuwa inaongoza bado asingeweza kujitapa sababu safari bado ndefu.

Pablo alisema anakubali kwamba Yanga ni timu nzuri na wanaongoza ligi lakini hiyo siyo sababu ya kwamba ndio watakuwa mabingwa msimu huu, sababu ligi inaushindani mkubwa lakini hata idadi ya pointi kutoka timu moja kwenda nyingine ni ndogo hivyo safari bado ni ndefu kwawote.

Alisema yeye na jeshi lake mikakati yao nikuhakikisha wanashinda kila mchezo wao wa ligi ili kuendelea kutoa presha kwa vinara Yanga, lengo likiwa ni kuwapita na kutetea ubingwa kwa msimu mwingine wa tano.

Aidha kocha huyo alisema katika kipindi hiki cha usajili amepanga kuongeza wachezaji watatu wapya kwa ajili ya kuimarisha sehemu zenye mapungufu jambo ambalo litakiongezea nguvu kikosi chake katika kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

Simba ni miongoni mwa timu tatu ambazo hazijapoteza mchezo kwenye mbio za Ligi Kuu ya Tanzania Bara, nyingine ni Yanga na Mbeya City.

Chanzo: Habarileo