Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PICHA: Coutinho karudi Liverpool leo

2208 48B249A200000578 5325589 Image A 46 1517237920510 634x400

Tue, 30 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil ambaye amecheza Liverpool ya England kwa kipindi cha miaka mitano Philippe Coutinho lakini katika kipindi cha dirisha dogo cha majira ya usajili cha mwezi January alitangazwa kujiunga na FC Barcelona ya Hispania.



Leo Jumatatu ya January 29 2018 Coutinho ameripotiwa kurudi katika jiji la Liverpool na kwenda kuaga ikiwa ni siku 21 zimepita aondoke England na kwenda Hispania kujiunga na FC Barcelona, imeripotiwa kuwa Coutinho amerudi katika jiji la Liverpool na kwenda katika uwanja wa mazoezi wa Liverpool Melwood kuaga marafiki zake.

Coutinho baada ya kurejea Liverpool Melwood alipokea na kukaribishwa na Adam Lallana ambaye walicheza pamoja nae toka 2014, kama utakuwa unakumbuka vizuri Coutinho amejiunga na FC Barcelona ya Hispania kwa uhamisho wa dau la pound milioni 145.

VIDEO: Magoli ya John Bocco na Okwi yalivyoiua Majimaji FC leo

Chanzo: millardayo.com