Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Oscar Oscar aagwa EFM, ataibukia wapi?

Efmtanzania 287449928 339762401569899 811540833662054080 N Oscar Oscar

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: EFM

Mchambuzi mwenye vituko vingi Bongo, Oscar Oscar au unaweza kumuita Mzee wa Kaliua, ameagwa rasmi na kituo chake cha EFM alichokuwa anafanyia kazi.

Kupitia ukurasa wao rasmi, EFM wameweka picha ya mchambuzi huyo yenye kichwa cha habari kilichosomeka:"Asante Mzee wa Kaliua Miaka 7 sio mchezo"

Kisha wakasindikiza na ujumbe huu: @oscaroscarjr ni mmoja wachambuzi waandamizi ambao wamekuwa nasi kwenye Sports HQ kwa miaka 7 sasa.

Sisi tunamshukuru kwa uchambuzi wa kina, vituko, maoni na yote aliyofanya kwenye kipindi hicho. Tunamtakia kila lenye kheri kwenye majukumu yake mapya.

Bado haijajulikani mchambuzi huyo ataibukia wapi, tusubiri tutaona!

Chanzo: EFM