Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Olimpiki 2024: Amchumbia mpenzi wake kwa pini

Pini Pict Olimpiki 2024: Amchumbia mpenzi wake kwa pini

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo kutoka Ufaransa ambaye ni mchezaji wa mchezo wa kuruka viunzi wa mbio za mita 3000, Alice Finot aliamua kuomba kuolewa na mpenzi mara baada ya kuvunja rekodi ya Ulaya Jumanne ya wiki iliyopita katika mashindano ya Olimpiki.

Finot alimaliza katika nafasi ya nne katika mashindano hayo ya mita 3000 yaliyokuwa na ushindani mkubwa ambapo bingwa wa dunia alikuwa ni Winfred Yavi kutoka Bahrain, lakini yeye aliweka rekodi ya kumaliza ndani ya dakika nane na sekunde 58.67. ndani ya Stade de France.

Baada ya kumalizika tu kwa mbio hizo, Alice mwenye umri wa miaka 33, alikimbia hadi jukwaani kwa ajili ya kumaliza shughuli nyingine.

Alipofika jukwaani alimkumbatia mpenzi wake ambaye pia ni mwanariadha Bruno Martinez Bargiela kisha akapiga goti na kutoa pini aliyokuwa amefunga namba yake ya ushiriki kwenye jezi yake kisha akapiga goti na kuomba kuolewa.

"Nilijiambia kwamba ikiwa ningekimbia chini ya dakika tisa ningefanya hicho nilichofanya, nilisema hivyo kwa sababu namba tisa ni nambari yangu ya bahati na kubwa zaidi tumekuwa pamoja kwa miaka tisa," alisema Finot alipoulizwa juu ya tukio hilo.

"Sipendi kufanya mambo yangu vile ambavyo watu wengine hufanya, kwamba (hajamvalisha pete), nilijiambia labda ni juu yangu kumvalisha, kwa hiyo, nilitoa pini ambayo nilikimbia nayo na kumpa mpenzi wangu, yeye ndiye anayenipa nguvu kila mara. Ilikuwa ni muda kidogo tu kupata medali lakini sijutii chochote kwa kukosa."

Wawili hawa wanakuwa ni wachumba wengine kuchumbiana katika mashindano haya ya Olimpiki baada ya wapendanao kutoka China ambao ni wachezaji wa mchezo badminton, Huang Ya Qiong na Liu Yuchen kufungua dimba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live